Huwezi kujiita mwanamme kama hujui kama nguo walizovaa wanao pesa imetoka wapi?
Huwezi kujiita mwanamme kama hujui nguo aliyovaa mkeo, nywele alizosuka na kila kitu chake kimetoka wapi?
Mkeo kufanya kazi sio tiketi ya wewe kugeuka kuwa mwanamme suruali?
Kuna watu wengine hujisahau eti kisa mke
anafanya kazi basi unafurahia kula kuku kila siku. Hata hujiongezi
ukatoa matumizi ya ndani?
Ungekuwa na akili kidogo ungejua kuwa
mshahara wa mkeo hautoshi kufanya vyote hivyo anavyofanya na ungekuwa
makini, sasa wewe unaridhika tu kwakuwa anafanya kazi unamuachia kazi ya
kuwa mwanamme.
Nikuambia tu kitu kimoja mwanamke hata
awe na pesa vipi bado anahitaji mwanamme wa kumtunza, yaani mtu wa
kwenda kumlalamikia shida zake na kumsikiliza. Sio kwenda kulalamikia
shida zake kwenye ATM.
Katika familia mwanamme unatakiwa kutoa
na mke kuchangia kwamba, hata kama ana kipato kikubwa lakini usibweteke
na kumuachia kila kitu, asipoweza kulalamika kwako atatafuta sehemu ya
kulalamikia.
Mwanamke anatakiwa kuongezea kilichopungua na si kutoa kisichokuepo.
Very true.
ReplyDeleteHayo maisha ni ya kizamaaaniiiii. Kwa sasa hivi zile Financial obligations ni equal. Hakuna cha mwanamke wala mwanaume. Ni lazima wote wawili wawajibike katika kuleta neema ndani ya nyumba yao. Ukiona mmojawapo anakuwa tegemezi kwa mwenzake kwa asilimia 100 ujue hapo hakuna kitu.
ReplyDelete