Binti wa aliyekuwa Mbunge wa
Mafia, Abdulkarim Shaa (CCM), Naima Shaa amezua balaa kwa mara nyingine
baada ya kunaswa akijiachia kwa mapozi ‘tata’ na golikipa namba moja wa
Timu ya Mtibwa Sugar, Saidi Mohamed ‘Nduda’.
Tukio
hilo lililoacha gumzo kwa muda lilijiri katika Ukumbi wa Maisha
Basement, Kijitonyama, Dar ambapo wawili hao walikuwa wamekwenda
kustarehe.
Kwa kamera ya shushushu wetu, Nduda
alifika ukumbini hapo akiwa na washkaji zake na Naima naye alikuwa
kivyake lakini walipokutana hali ilibadilika na kuanza kufanya yao.Naima Shaa akiwa na Manyika JR
“Walionesha kama watu waliomisiana
kitambo. Nduda alipomuona Naima tu, alimfuata harakaharaka na kuanza
kupiga naye mapicha tata kabla ya kukumbatiana na kuzungumza kwa muda
huku wengine wakisema kuwa ni mrithi wa aliyekuwa mpenzi wa mwanadada
huyo ambaye ni kipa wa Simba, Peter Manyika Jr,”“Baada ya kujiachia kwa mapichapicha, wawili hao walipoulizwa kama kwa sasa ni wapenzi hawakuwa tayari kufunguka. alifunguka shushushu wetu na kuongeza:“Zaidi
sana waliendelea kuburudika kwa muda kabla ya mwishoni kabisa kutokana
na wingi wa watu waliokuwemo ukumbini hapo, haikujulikana mara moja kama
waliondoka pamoja.”
Naima
ambaye aliwahi kuwa mke wa mfanyabiashara wa jijini Dar, Mwanamboka,
aliwahi kuripotiwa kumzidi kete aliyekuwa shosti wake, Wema Isaac Sepetu
na kudaiwa kumpora kigogo wake aliyekuwa maarufu kwa jina la CK.Mbali
na hilo, pia aliwahi kuripotiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii
wa Bongo Fleva, Aslay Isihaka ‘Dogo Aslay’ hadi kujichora tatuu ya
msanii huyo. Baada ya kuachana na Dogo Aslay, Naima alitumbukia kwenye
penzi la Peter Manyika Jr kabla ya uhusiano wao kukata kamba miezi
kadhaa iliyopita.