RAIS Uhuru Kenyatta amezindua sehemu ya tatu ya mahari ya polisi na
vifaa vilivyopatikana kupitia mpango wa kukodi wa serikali.
Kenyatta amezindya magari 525, yakiwemo 25 maalumu kwa ajili ya
kujilinda na mabomu ya kutegwa ardhini ama Mine-Resistant Ambush
Protected (MRAP), huko Uhuru Park Nairobi, kama sehemu ya mpango wa
serikali kulifanya jeshi la polisi la nchi hiyo kuwa la kisasa.
Katika hotuba yake, rais huyo wa Kenya alirudia dhamira ya serikali
yake katika kuimarisha mazingira ya kazi ya polisi na maafisa wengine wa
usalama.
Baadhi ya magari yalikopwa kutoka kampuni ya General Motors East Africa, ambayo itahusika katika kuyahudumia magari hayo.
Magari mengine 500 yanategemewa kuwasaidia polisi katika kazi zao za kila siku katika kaunti, na mijini.
Jumla ya magari 2,220 yalizinduliwa wakati wa awamu ya kwanza nay a pili ya mpango huo.
Hatua hii ina lengo la kuimarisha doria ya polisi kwa kuwapa magari, pamoja na njia nyingine za usafiri.
African countries terrible. This shows that the election won't be free and fair. The commanding these forces will win. What is behind these cars?
ReplyDelete