Madawati yawaweka mtegoni wakuu wa mikoa saba

Dar\mikoani. Wakuu wa mikoa saba nchini wanapambana kulinda ajira zao kwa kuhakikisha wanatatua tatizo la upungufu wa madawati baada ya kupewa siku 43 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene.

Wakuu hao wa mikoa ya Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma walipewa siku hizo na Simbachawene wawe wametatua tatizo la upungufu wa madawati katika mikoa yao baada ya kuonekana ina upungufu.

Agizo hilo alilitoa Novemba 18, mwaka jana akieleza kushindwa kulitekeleza katika siku hizo watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Rais John Magufuli.

Alitoa siku hizo baada ya kupokea madawati 3,500 yenye thamani ya Sh300 milioni kutoka Benki ya NMB.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad