Mahakama Kuu
Divisheni ya Biashara imeiamuru kampuni ya Uingereza yenye makao yake
Kenya, British American Tobacco Kenya Limited (BAT), kuilipa fidia ya
Sh6.2 bilioni kampuni ya Mohan’s Oysterbay Drinks Limited ya nchini.
Uamuzi huo unatokana na Mahakama kuridhika kuwa kulikuwa na makubaliano ya kibiashara kati ya Mohan’s na BAT ambayo iliyavunja.
Mohan’s
iliomba kulipwa Sh12 bilioni zikiwa ni fidia ya uwekezaji iliofanya
kutokana na makubaliano hayo, hasara ya kibiashara, faida
waliyoitarajia, hasara ya jumla na riba. Makubaliano hayo yalihusu
usambazaji wa sigara zinazozalishwa na BAT aina ya Dunhill na Benson
& Hedges.
BAT
ilikana kuwa na uhusiano wa kibiashara na Mohan’s kama msambazaji wa
bidhaa zake kwa madai kuwa hapakuwa na mkataba wa maandishi, bali
uhusianao wao ulikuwa ni muuzaji na mnunuzi.
Jaji
Latifa Mansoor katika hukumu ya kesi hiyo, amesema vielelezo
vilivyowasilishwa na Mohan’s mahakamani vinabainisha kulikuwa na
makubaliano ya kibiashara ya mtengenezaji na msambazaji na si muuzaji na
mnunuzi.
Amesema
BAT haikuwa na sababu ya msingi kuvunja makubaliano kwa kuwa
haikuonyesha kuwa Mohan’s ilitenda kosa la ukiukaji wa makubaliano
lililosababisha kuyasitisha baada ya kuwapo uhusiano wa kibiashara wa
miaka 19.
Jaji
Mansoor amesema BAT ingeweza kujadiliana na Mohan’s kuhusu masharti
yenye manufaa kwa makubaliano ya usambaji bidhaa hizo, huku wakiweka
kifungu cha kuyasitisha jambo ambalo lingewezesha kuendeleza biashara
kwa muda mrefu.
Licha
ya kukubaliana na madai ya Mohan’s kuhusu uhusiano wake na BAT, hata
hivyo Jaji Mansoor hakukubaliana na kiwango cha fidia ambacho kampuni
hiyo ya Mohan’s ilikuwa imekiomba cha Sh12,079,000,000.
Badala
yake Jaji Mansoor ameamuru kampuni hiyo ya BAT kuilipa Mohan’s fidia ya
jumla ya Sh6,234,835,855 (zaidi ya Sh6.2 bilioni), ikiwa ni fidia ya
hasara ya gharama za uwekezaji, hasara ya kibiashara, hasara ya jumla,
Pia
ameiamuru BAT kulipa asilimia 12 ya kiasi hicho tangu siku ya hukumu
hadi itakapokamilisha malipo hayo na pia kulipa gharama zote za kesi
hiyo.
Jaji
amesema katika hukumu hiyo kuwa kampuni hiyo imeshindwa kuthibitisha
madai mengine kiasi cha Sh12 bilioni ilichokuwa ikiomba, kama vile
mapato ya mauzo waliyokuwa wakiyatarajia, malipo ya fidia na malipo ya
bima kwa wafanyakazi waliowapunguza.
Mohan’s
kupitia kwa Wakili wake Dillip Kesaria ililieleza Mwananchi kuwa ingawa
madai yake ya fidia ya zaidi ya Sh12 bilioni iliyokuwa ikiiomba
hayakukubaliwa, lakini wameridhika na hukumu hiyo na kiasi cha zaidi ya
Sh6.2 bilioni walizopewa na Mahakama.
Wakati
Mohan’s ikieelezea kuridhika na hukumu hiyo, BAT kwa upande wake
kupitia kwa Wakili wake, Karume, ililieleza kuwa haikuridhika na hukumu
hiyo na kwamba itakata rufaa katika Mahakama ya Rufani kuipinga.
Wakili
Karume alibainisha kuwa tayari wameshachukua hatua za awali za kukata
rufaa kuipinga hukumu hiyo, kwa kuwasilisha mahakamani taarifa ya
kusudio la kukata rufaa.
“Hivyo
kwa sasa tunasubiri tu kupata mwenendo wa kesi hiyo ili tuweze kukata
rufaa rasmi kwa kuwasilisha mahakamani sababu za rufaa yetu,”amesema
Wakili Karume.
Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa