MANENO ya dogo aliyetangazwa ‘man of the match’ vs Yanga


Nimefanikiwa kufanya mazungumzo mafupi na kijana mdogo Greyson Gerald ambaye alitangazwa kuwa man of the match wa mechi kati ya Yanga dhidi ya Jamhuri .

Licha ya timu yake kupoteza kwa idadi kubwa ya magoli (ilifungwa 6-0) kijana huyu anavalia jezi namba 6 kwenye kikosi cha Jamhuri alikuwa bora katika mchezo huo kwa kuonesha kiwango bora katika eneo la kiungo licha ya kupambana na wachezaji wakongwe na wazoefu kama Kamusoko, Zulu, Niyonzima na wengine wengi.

Nashawishika kumuuliza nini hasa kilichopelekea utulivu wake uwanjani na kujiamini mbele ya Yanga ambayo ndio mara ya kwanza alikuwa anakutana nayo tangu alipoanza kucheza soka.

Sikuwa na presha kabisa, niliona ni kawaida licha ya kucheza na timu kubwa,” anasema Greyson ambaye anaitumikia Jamhuri kwa msimu wa pili.

Kinda huyo ambaye aling’ara mbele ya mibaba ya Yanga anasema alianza kucheza ligi daraja la kwanza akiwa na Kurugenzi ya Mafinga, Iringa alipocheza kwa msimu mmoja kabla ya kuvuka maji na kujiunga na Jamhuri ya visiwani Zanzibar.

“Najisikia furaha kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo dhidi ya Yanga, lakini kwa idadi ya magoli tuliyofungwa leo nadhani ilikuwa ni presha kwa wachezaji wenzangu kwa sababu tulikuwa tunacheza na timu kubwa kwahiyo wakapoteza kujiamini.”

Watu wengi huenda wanadhani dogo ni mzaliwa wa Zanzibar, lakini kumbe anatokea Ifakara mkoani Morogoro: “Mimi ni mzaliwa wa Ifakara, Kilombero mkoani Morogoro.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad