Maskini… Snura alizwa na mwanaye ..!!!


MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara, Snura Mushi, amefunguka kuwa amekuwa akilizwa kila mara na mtoto wake wa kwanza Talha, kutokana na maneno anayomueleza kwa kitendo cha baba yake kutompa huduma yoyote.


Akizungumza  Snura alisema kila mara mtoto wake anamuambia asikate tamaa ya kuwalea na kumuombea kwa Mungu, aweze kumsaidia ili waendelee kusoma na kupata huduma japo baba zao hawawajali yeye na mdogo wake kitu kinachomliza mara kwa mara.

“Yaani nasikiaga maumivu makali sana  mtoto wangu mdogo wa miaka sita tu ananiambia maneno hayo yananiumiza kuliko kitu chochote kile huwa yananifanya nijitahidi kila kukicha ili nisimuangushe na nitaendelea kukatika ili mtoto wangu apate elimu aitakayo,” alisema Snura ambaye amezalishwa watoto wawili na baba tofauti.

Download Application ya Udaku Special Blog Kwa Kubonyeza Hapa


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad