UKUMUANGALIA tu lazima ucheke kwani ni kipaji na sio ngekewa,
amefanikiwa kuteka watoto, vijana, watu wazima na wazee hiyo yote ni
kutokana na kuigiza nyanja zote tena bila wasiwasi wowote ule, Lucas
Mhavile maarufu Joti alitamba na Original Comedy kundi ambalo lilitoa
burudani kwa muda wa miaka 11 bila kuwa na mpinzani katika angaza za
uchekeshaji wenye mafundisho.
Kwa sasa kampuni yao imepumzika na kila mmoja kufanya shughuli zake
ili kutoa fursa kwa vizazi vipya kuonyesha kazi zao, Kwa upande wake
Joti ameamua kutumia mapumziko yake kwa kuanzisha Yotube Tv akiamini
sasa hivi dunia iko kwenye kiganja.
“Nimeamua kuanzisha Yotube Tv kwa sababu dunia iko kwenye kiganja
watu wanakosa muda wa kuangalia Tv, ila akiwa na simu yake ya mkononi
anawez kuona chochote kile anachotaka hata kama ni saa sita usiku akiwa
kitandani uwezo wa kumuangalia Joti upo.”
Tv hiyo imelenga nyanja zote na imeangalia sana watoto kwa sababu
kitu akikipenda mtoto basi na mzazi atakipenda, pia kutoa elimu kwa
watoto katika uchekeshaji wangu huo nitatoa elimu kwa watoto na mambo
mengine mengi makubwa ya watoto yanakuja.
Watoto ni watu ambao wanaupendo wa kweli hawana unafiki na ndio
vipaji ambavyo vinatakiwa kuendeleza kwa kuliona hilo nikaona hamna haja
ya kuacha vipaji vyenye upendo wa kweli vipotee ni bora niwe navyo bega
kwa bega.
“Licha ya kuegemea zaidi katika vipindi vya watoto, nitakuwa na
vipindi vya watu wa rika zote pia nitatoa ajira kwa vijana wenzangu kwa
sababu sita weza kufanya kazi peke yangu.
Hata hivyo Joti alifafanua kuwa Chaneli yake itahusika na shughuli
zake pekee mtu asitegemee kuona taarifa za habari na mambo mengine kama
chanel za watu wengine.
Aidha Joti alisema kuna wachekeshaji wengi chipukizi wanafanya vizuri
ila hawataki ushauri, wala hawana mtu waliyempenda ili kuingia katika
hiyo kazi hili nitatizo na mtu kuwa staa lazima uwe na historia huwezi
kukurupuka na kuwa staa.
“Mimi nimepitia analogi na digital na nimejua vitu vingi kwa kuwa
nilipitia kote ninauwezo wa kuutunza ustaa wangu hata miaka 15 ijayo kwa
sababu najua kwenda na wakati, tatizo liko kwa vijana wanaochipukia
wanataka kuwa Digital tu, pia hawana historia, hawashauriki ndipo
tunapowaangalia na kwa sababu najua vurugu zake zote lazima akutane na
ukuta na mimi simu yangu iko wazi muda wowote kwa anayetaka ushauri
kutoka kwangu.”
Sikufahamu kama ninakipaji ila King Majuto ndio sababu amenipotezea
sana muda, na amekula sana hela zangu wakati huo nilikuwa nikiona kuna
onyesho lake shuleni basi lazma niingie, pia kumuangalia kwenye tv,
lazima nipoteze muda kumuangalia hadi linikuwa nikipigwa sana na wazazi
wangu kumbe ni kitu ambacho nilikuwa nakuja kukifanya ndio maana
nilikuwa nakifuatilia sana ila bila kujua kama nitakuja kuwa
mchekeshaji.
“Napita kwenye ugumu mwingi sana, kwa sababu unaweza ukapita sehemu
mtu mmoja akakuomba kupiga picha ukakubali basi wataibuka wengine hapo
hata 30 na huwezi kukataa ukikataa hata kama unachelewa utasikia
wanasema supa staa Bongo neno ambalo naliogopa sana katika maisha yangu
kwani hao wanaosema hivyo ndiyo mashabiki wangu wa wanaweza kunipandisha
au kunishusha.’