Mkuu wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Gabriel Simon Mnyele amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Januari 26, 2017 na kuwaaga madiwani wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano alioufanya wilayani humo.
Akieleza sababu ya kufanya uamuzi huo, Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa alimwandikia Rais Dkt Magufuli barua ya kujiuzulu nafasi hiyo akielezea kusongwa na majukumu binafsi.
Mkuu wa Wilaya, Gabriel Simon Mnyele alikuwa miongoni mwa Wakuu wa Wilaya 139 walioteuliwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli tarehe 26 Juni, 2016.
Cheza na Magufuli wewe. Na bado. Wengi tu mtamfuata.
ReplyDeleteWe anonymous 2.27 sikuelewi
ReplyDeleteWeee!!!!nawe umwelewi vip? Mziki wa baba Magu. Mnene sio mchezo kama hauendani na hapa kazi tu. Weee tangu lini? Ukaona mtu anapewa madaraka serikalini alafu akayachia ilikuwa ni huko nyuma kwenye uongozi wa mama nibebe lakini sio baba Magu. Ni kazi tu. Hakuna madili wala ufisadi wala rushwa ni mwendo mdundo tu wa mchaka mchaka. Sio mchezo
Delete