Msajili wa Siasa Aibuka na Mapya Juu ya Cuf...!!!!

 
OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa, imesisitiza msimamo wake  kwamba Chama cha Wananchi (CUF) ni kimoja, hivyo yeyote mwenye malalamiko ayapeleke ofisini ili yashughulikiwe na si kulalamika kupitia vyombo vya habari.

Kauli hiyo imekuja baada ya  mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, Julius Mtatiro kueleza jinsi Profesa Ibrahim Lipumba alivyochukua fedha za ruzuku zaidi ya shilingi milioni 369 kutoka Hazina.

Mtatiro anamtaja msajili, Jaji Francis Mutungi kuwa anafahamu na kuidhinisha mchakato huo wakati Oktoba 10 mwaka jana, aliandika barua ya kusitisha utoaji wa ruzuku kwa chama hicho kutokana na mgogoro hadi hali itakapokuwa shwari kiutendaji.

Lakini mwishoni mwa juma, mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano katika ofisi hiyo ya Msajili, Monica Laurent alieleza kuwa kuna chama kimoja tu cha CUF.

“Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inatambua CUF iko moja tu, Kama CUF kuna watu wana malalamiko ya msingi wayalete rasmi ofisini, huo ndiyo msimamo wetu,” alisema Laurent.

Aidha aliwataka kutumia mfumo rasmi wa kuwasilisha malalamiko hayo kwenye ofisi ya msajili, akibainisha kuwa ofisi hiyo haiwezi kujibu masuala hayo kwenye vyombo vya habari.

Hivi karibuni Mtatiro akizungumza na vyombo vya habari alieleza kuwa tangu Msajili aandike barua ya kusitisha ruzuku, chama kinadai Hazina sh. 635 Milioni, hivyo CUF haitambui  utaratibu mwingine uliotumika kuigawa ruzuku hiyo hadi Lipumba akapata mgawo wake.

Alisema chama kimeibiwa fedha za ruzuku sh. 369 ambazo zilitoroshwa kutoka Hazina ya Serikali Kuu Januari 5 na kuingizwa kwenye akaunti ya NMB tawi la Temeke yenye jina la The Civic United Front, ikiwa ni akaunti namba 2072300456.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad