Klabu ya Young Africans Sports Club alimaarufu kama Yanga ambayo
ilishiriki katika michuano ya 11 Kombe la Mapinduzi ambayo imemalizika
jana kwa Azam FC kuibuka mabingwa baada ya kuwalaza bao 1-0 Simba SC.
Yanga
imeamua kumtunuku ngao ya ushujaa kiungo, wimba na mshambuliaji wake wa
pembeni Saimoni Msuva kutokana na mchango wake mkubwa katika klabu hiyo
pia Msuva ameibuka kuwa mfungaji bora wa timu hiyo katika michuano ya
Kombe la Mapinduzi baada ya kutupia jumla ya magoli 4 mbali ya goli hizo
katika jumla ya magoli 8 ambayo Yanga imepata nje ya magoli 2 ya
matuta, Msuva ametoa usaidizi ya magoli 2.
"Msuva amekuwa mchezaji tegemeo kwenye timu katika michuano
mbalimbali inayoshiriki klabu hali inayomfanya kusimama kama ngao muhimu
ya ushindi. Kasi yake, utulivu na kufuata maelekezo ya waalimu wake
vinamfanya kuwa bora kila uchao. Kubwa zaidi kwa mchezaji huyu ni
nidhamu binafsi,uelewano mzuri na wenzake, ucheshi na moyo wa kujituma
muda wote vinamfanya kung'ara kila uchao". Yanga