MUKANDALA: UDSM Haijaathirika Kwa Teuzi za Rais Kwa Wanataaluma wake

Rais J.P Magufuli amekuwa akiteua wanaataluma kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) hali.iliyopelekea baadhi ya watu kuhoji kama teuzi hizo hazitaathiri uwezo wa chuo hicho kitaaluma.

Akitolea ufafanuzi suala hilo Makamu Mkuu (Deputy Chancellor) Profesa Rwekaza Mukandala amesema kuwa teuzi hizo hazijaathiri chuo hicho kikongwe katika taaluma. Aliongeza kuwa chuo kina uwezo wa kuzalisha rasilimali watu kwa kiwango kikubwa hivyo teuzi chache kwa nafasi mbalimbali katika serikali kuu haziwezi kuathiri chuo.

"Chuo kikuu cha Dar es salaam na serikali vina historia ya mashirikiano kwa miaka mingi na lengo hasa la kuanzishwa kwa chuo hiki ni kuzalisha na kufundisha wataalamu katika nyanja tofauti ili watumike serikalini" alisema Mukandala.
Hivi karibuni rais Magufuli alimteua Dr Tito Esau Mwinuka kuwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO.

Teuzi nyingine zilizofanywa na Rais kwa wanataaluma kutoka UDSM ni kama ifuatavyo:

1. Prof Godius Kahyarara - DG NSSF
2. Prof EGID MUBOFU - DG TBS
3. Prof Adolf Mkenda - PS wizara ya Viwanda na biashara
4. Justine Ntalikwa - Wizara ya Nishati na Madini
5. Dr John Njigu - Mwenyekiti NEEC
6. Dr Ayoub Ryoba - DG TBC
7. Prof Longinusi Rutasitara - Mshauri wa Rais masuala ya kiuchumi

Kwa kumbukumbu tu: UDSM ina wanataaluma wenye Phd wapatao 600.

Wapo wanaohisi kuwa UDSM ndio chanzo cha Think Tank ya Tanzania.
Mafanikio ya wanataaluma hawa katika nyadhifa ni jambo linalohitaji mjadala tofauti na huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad