Mwana wa Rais Yoweri Museveni, Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba na mkewe Charlotte Kutesa Kainerugaba alipokuwa anapandishwa cheo kuwa meja jenerali Mei 25, 2016.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amemteua mwanawe Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba, kuwa mshauri mkuu wa rais kuhusu operesheni maalum.
Mke wa Museveni, Bi Janet Kataaha Museveni ni Waziri wa Elimu na Michezo, wadhifa ambao alikabidhiwa Juni mwaka jana.
Jenerali Kainerugaba amekuwa kamanda wa kikosi maalum cha wanajeshi (SFC) chenye jukumu la kutekeleza operesheni maalum za kijeshi.
Kikosi hicho husimamia ulinzi wa rais na kulinda maeneo muhimu kwa serikali Uganda.
Luteni kanali Don Nabaasa amepandishwa cheo na kuwa kanali na akateuliwa kaimu kamanda wa SFC.
Rais Museveni pia amemteua mkuu mpya wa majeshi, Meja Jenerali David Muhoozi ambaye amepandishwa cheo na kuwa jenerali.
Mkuu wa majeshi wa awali, Jenerali Edward Katumba Wamala amehamishwa na kuteuliwa waziri wa ujenzi.
Meja Jenerali Muhoozi Kainerugaba (kati) amekuwa kamanda wa kikosi maalum Uganda
Kwenye mabadiliko hayo yaliyotangazwa na msemaji wa Majeshi ya Ulinzi ya Uganda (UPDF)
Luteni Kanali, Rais Museveni amempandisha afisa mkuu wa majeshi aliyeongoza operesheni ya kushambulia ikulu ya mfalme wa Rwenzururu, magharibi mwa nchi hiyo.
Watu 100 walifariki wakati wa operesheni hiyo. Mfalme wa Rwenzururu Charles Wesley Mumbere alikamatwa na bado anazuiliwa
Brigidia Peter Elwelu, aliyekuwa mkuu wa kikosi cha wanajeshi hao wenye kambi yao kuu Mbarara, amepandishwa cheo na kuwa meja jenerali na akateuliwa kamanda wa majeshi ya nchi kavu.
Udugunasition aliokuwa akiupigaga vita Nyerere watu wakawa hawamuelewi unampa wewe rais unampa uwaziri mkeo na unampa ujenerali mtoto wako kesho naona utamteua shangazi yako awe spika wa bunge kadhalika na kadhalika haĺafu mwishoni unaita hiyo ni demokrasi utawala wa kimwinyi na mabavu Africa hauwezi kuisha kamwe mliwafukuza wakoloni mkadai uhuru sasa uhuru mmeishaupata badala ya kusaidiana viongozi hao hao waliokuwa wanasema mkoloni anatugandamiza wao hao hao wamekuwa wanawagandamiza waafrika wenzao bila ya aibu na huruma kupita hao wakoloni
ReplyDeleteWAGANDA WATABULUZWA MPAKA BASI,KM IDDY AMINI(R.I.P) TU HAMNA TOFAUTI YYTE..WAGANDA AMKENIIIIIIIII..MMELALA SAAAANA..NDIYO MADHARA YA ndiyo mzee HIYO..NA BADO..
ReplyDeleteNdio maana zari amekimbia ....kwa mambo hayo ya ndio mzee
ReplyDelete