Mwana FA Afungukia Bifu Lake na Lady Jay Dee.....

Mwanamuziki Hamis Mwinjuma maarufu Mwana FA au Binamu akifanya mahojiano siku za karibuni jijini Dar es Salaam amezungumzia tofauti kati yake na mwanamuziki mwenzake Judith Wambura maarufu Lady JayDee.

Mwana FA alisema kuwa yeye hana tatizo lolote na Lady JayDee na wala wawili hao hawajawahi kukutana kisha mmoja akamwambia mwenzake kuwa anatatizo na mwingine.

“Kila mtu anafanya shughuli zake na mimi sijawahi kumwambia chochote sababu sina tatizo na yeye, kwa hiyo sioni kama kuna haja ya kupatanishwa sababu naona kila mtu anafanya shughuli zake” alisema Mwana FA.

Mwana FA alisema kuwa kwa sasa yeye na mwanamuziki huyo hawapo karibu kama walivyokuwa kipindi cha nyuma lakini anaamini hakuna tatizo ni kila mtu tu ameamua kufanya kazi zake kivyake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad