Mwanamke wa Kitanzania Akamatwa na Mzigo wa Madawa ya Kulevya Tumboni


INDONESIA: Mwanamke Mtanzania akamatwa akiwa na Wanigeria wawili wakijaribu kuingiza mihadarati. Mnigeria mmoja ameuawa akijaribu kutoroka. Mtanzania huyo alikamatwa siku ya jumatano katika Jiji la Jakarta.

Baada ya upekuzi Mtanzania huyo akutwa na gramu 138 za Crystal Methamphetamine, kete nyingine 66 za Crystal Methamphetamine alikuwa amezimeza na gramu 3 za bangi alizoficha kwenye nguo yake ya ndani.

Wakati huo huo, polisi nchini Namibia wanadai kukamata watu 135 kati ya Novemba 1 na Disemba 2016 kwa tuhuma za dawa za kulevya aina ya Mandrax, Cocaine, Crack Cocaine, Heroin na Bangi. Kati ya waliokamatwa na dawa hizo wapo Watanzania watano.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. amekamatwa indonesia huyo atanyongwa kuna watu wawili kutoka Australia na mwingine kutoka Nigeria walikamatwa na madawa wakanyongwa si muda mrefu umepita

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad