MWANAMUZIKI Darassa Afunguka "Diamond Hapaswi Kujiita Simba"

Msanii wa bongo fleva Darasa ameweka wazi ule mstari wake wa "sio simba, sio chui, sio mamba" kwa kusema Diamond hakupaswa kujiita simba kwani simba ni mnyama ambaye anaweza kuuliwa anapozidiwa nguvu.

Akipiga story kupitia eNewz Darasa amesema Diamond ni msanii ambaye amehangaika sana kutoka kimuziki hivyo mafanikio yake na uwezo wake wa muziki alitakiwa ajiite jina lingine kwa kuwa Daimondi ni zaidi ya Simba kwa sasa kwani ni zaidi ya mnyama Simba.

"Ningekuwa Diamond nisingejiita simba, ninavyomuona Diamond ni zaidi ya Simba, kuna watu wanaua simba, simba, kajichanganya, kaingia kijijini kapotea, Diamond kwa kitu anachofanya ni zaidi ya simba, angeweza kujiita jina lingine lolote kubwa, kafanya vitu vingi sana". Amesema Darassa


Darassa amemalizia kwa kusema wanyama wote ambao amewataja katika wimbo wake hawaogopi kwa kuwa ana kitu kikubwa ndani yake na yeye ni mwanaume na anajiamini kwa muziki wake anaofanya.

"Kwa upande wangu nimesema siyo simba, siyo chui siyo mamba, mamba ni mnyama anayetisha sana kwenye maji, simba anatisha sana porini, chui ni hunter mzuri, so katika vitu vyote ambavyo viko humo, mimi humo kote simo, ninacho kitu ambacho kinaweza kunifanya nikwambie aaaaah". Amemalizia Darassa
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. kuna yule mnyama pori sijui anaitwa nyati na yule pia ni kiboko kwa simba pale simba akimjia karibu nyati anampiga kichwa simba na mapembe yake halafu simba anaangukia kule mbali kule ha ha ha nyati anayo mapembe lakini simba hana

    ReplyDelete
  2. Hongera sana DARASSA FUNIKA BOVUU,DIAMOND HAKUWEZIII TUPA KULEEE!! UKO JUU SIO MCHEZOOO TUMECHOKA MUZIKI WA UJANJA UJANJAAA 👍🏾ILA ANGALIA DIAMOND ASIJE KUKUROGAA KWA WIVU WAKEEE ANA ROHO MBAYAAA SAANAAA NI BORA UWE KARIBU NA ALIKIBA TUU👏🏾👌🏾HABARI NDIO HIYOOO👏🏾👏🏾👏🏾

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ukimjua mchawi, basi unawanga nae.......kawaida ya MCHAWI ANAMJUA MCHAWI MWENZIE........

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad