Mzee Jangala Awachana Wasanii wa Kiume Wanaovaa Nguo za Kubana na Kutoboa Masikio..!!!


Mkongwe wa sanaa za maigizo nchini Mzee Jangala amewachana wasanii wa kiume wanaovaa nguo zinazobana, kutoboa masikio na kuonesha maumbile yao.

Akiongea kupitia eNewz amesema vijana wanapaswa kujitambua na kuelewa maana ya utandawazi na siyo kuiga mambo mbalimbali ikiwemo kukaa uchi mbele za watu wazima kubadilisha maumbile yao halisi na kudai kuwa wanafuata utandawazi na kupotosha jamii zima.

Hata hivyo Mzee Jangala hakusita kuwasihi wasanii wa kizazi kipya kujitambua na kufanya mambo ya msingi katika jamii kwa kuwa wao ni watu ambao wana mashabiki ambao wanawaufatilia maisha yao na kuiga kila kinachofanywa na watu maarufu.
 

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sawa Kabisa mzee Jangala..Kujitambua vijana wetu ni kitu muhimu.. Kufata Maadili na utamaduni wetu havina Mbadala ni Lazina. ili tuweze kuwa na kizazi chenye mwamko na heshima baina yako na upendo ili tuweze kuwa na taifa jipya la Tanzania Mpya huko mbele. Chonde Chonde Vijana wetu wa sasa...Msikie ya wakuu.....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad