Namna Diamond Anavyoendelea Kulisadifu Jina lake la Utani ‘Simba’


Simba ni mnyama ambaye hulka yake ni kulinda himaya yake, na ni maarufu kwa jinsi anavyotumia nguvu kuhakiksha anapata akitakacho wakati wowote pahali popote. Hivyo huogopwa na kuheshimiwa na wanyama wenzake maana yeye huwa hana mzaha a biashara zake ilimradi tu ahakikishe jamii yake inafaidika kutoka kwa windo lake.



Huenda sifa za mnyama huyu ndizo zilizopelekea CEO wa WCB Naseeb Abdul Juma aka Diamond Platnumz kujiongezea jina la Simba kama moja aka zake. Kwa ubunifu wake wa hali ya juu, star huyo wa wimbo Salome hasiti kuwatoa kijasho wasanii wenzake kwa kasi zake, si kimziki pekee bali pia kibiashara.

Wakati wengi wakitaka kumpiku kisanaa kwa kutoa hits na video kali ili kuvutia mashabaki, yeye anazidi kutumia hela anazoingiza kupitia muziki wake kwa show anazopiga hapa Afrika hadi Ulaya kupanua himaya yake ya WCB kwa kujenga na kununua nyumba za kifahari ikiwemo moja nchini Afrika Kusini.

Nina hakika Afrika Kusini kama vile ilivyo hapa Afrika Mashariki kuna baadhi ya wasanii tajika ambao bado wanaishi katika nyumba za kupanga. Inatisha sana ukiona msanii kutoka nchi ya kigeni kama Tanzania akimiliki nyumba ya kifahari kwa thamani ya zaidi ya milioni 400 iliyopo katika jiji la Pretoria.

Juzi tu, meneja wake Sallam alitangaza kuingia sokoni wakati wowote lwa manukato ya Chibu Perfume ambayo mwaka jana 2016 sample zake zilionyeshwa kwa mara ya kwanza nakuwapa hamu ya kuzitumia mashabiki wake kote barani Afrika.

Wakati mashabaki wake wakiwa katika harakati za kushangilia ujio wa Chibu Perfume ndani ya soko la Afrkca, siku tano zilizopita Baba Tiffa alirusha video kupitia kichunusi chake cha Instagram akiwa anaonyesha furaha baada ya kusaini (endorsement deal ) ya mamilioni ya pesa japo hakuweka wazi kama deal hiyo ilikuwa imetoka kwa kampuni gani.

Baraka hizi zote lazima zinawapa homa na kichefuchefu wasanii wengi Afrika, kwani kila mmoja anapania kufikia upeo wa mafanikio hayo. Umaarufu wake barani Afrika na nje, unamfanya kuwa na kila sababu ya kumiliki aka yake ya Simba.

Mwaka ukiwa bado mchanga, ameanza na mbwembwe za kuuonyesha ulimwengu kuwa pia yeye ni star katika uwanja wa biashara na vigezo vya ujasirimali vimejitokeza wazi. Heko Chibu kwa juhudi unazopiga wewe. Wewe ni msanii kioo cha jamii, waonyeshe njia nzuri vijana wasiishie kwenye lindi la dawa za kulenya.

Makala ya: Changez Ndzai (Kenya)
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad