Ni Maajabu na Kizaazaa Mbeya:Mtoto Aliyezikwa Jana Akutwa Akiwa Amelala Chumbani Kwake,Tazama Video Hapa..!!


Wakazi wa eneo la Isanga katika jiji la Mbeya wameendelea kushuhudia visa na mikasa, ushilawadu na matukio ya vioja, baada ya mtoto wa miaka 9 aliyekuwa amezikwa jana kwenye makaburi ya Isanga kukutwa akiwa kitandani kwake amelala usingizi mara baada ya kurejea kutoka makaburini.


Mara baada ya kufika nyumbani familia ikiwa inaingia ndani mwao, walipigwa na butwaa baada ya kukuta mtoto wao amelala kitandani kwake, na baada ya kuitana na kumwamsha mtoto huyo aliamka na kuonekana akishangaa hali aliyoiona pale nyumbani.


Kwa pamoja wananchi na wanafamilia walikubaliana asubuhi hii kwenda kufukua kaburi hilo ili waone nini kilichozikwa, na hivi dakika hizi zoezi hilo linaendelea na picha za makabuni hapo .

UPDATES KUTOKA ENEO LA TUKIO

KABURI LIMEFUKULIWA, HAKUNA KILICHOKUTWA NDANI YA KABURI YAANI MAITI ILIYOZIKWA JANA HAIMO!! POLISI WAMELAZIMIKA KUPIGA MABOMU ILI KUTAWANYA WATU PALE MAKABURINI BAADA YA KUANZA HALI YA SINTOFAHAMU JUU YA NINI KIMETOKEA?

Kutoka katika kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM wamemuhoji Kamanda wa Polisi wa Jiji la Mbeya ambaye amatoa maelezo kuwa, ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuwa mwili wa mtoto huyo ulisahaulika kuwekwa katika sanduku na baada ya ibada mwili haukuagwa (Familia iliomba hivyo na ni kawaida).
Baada ya kuzika waliporudi nyumbani ndipo waliukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umelala kitandani. Jeshi la Polisi liliimarisha ulinzi katika maeneo hayo ya msiba.

Mmoja ya watangazaji wa Leo Tena amesema kuwa amewasiliana na mmoja ya wadau wake huko Mbeya na amemthibitishia kuwa kaburi limefukuliwa na jeneza limekutwa likiwa tupu halina kitu.

Inavyoonekana kuna uzembe katika kuandaa mwili na kuuweka katika jeneza, ingawa pia majirani na watu wanaoishi mazingira hayo wanahusisha na imani za kishirikina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad