Hakimu Mfawidhi wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, leo,
anatarajia kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless
Lema na mkewe, Neema katika kesi inayowakabili ya kumtukana Mkuu wa mkoa
huo, Mrisho Gambo.
Hoja
hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016 lakini zilikwama kusomwa
kutokana na Lema kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth Swai
kumuomba hakimu kutumia busara ya Mahakama kuisogeza mbele kesi hiyo
kutokana na hali ya mbunge huyo.
Lema
bado anasota rumande kwa siku 76 tangu Novemba 2, mwaka jana baada ya
kukosa dhamana katika kesi inayomkabili ya tuhuma za kutumia lugha ya
uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.
Kutokana
na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia amwahirisha kesi ya kuhamasisha
maandamano ya Ukuta inayomkabili mbunge huyo na ile ya kumtumia ujumbe
mfupi wa maneno Gambo unaodaiwa kuwa na matusi hadi leo.