Ningekuwa Rais ningewekeza kwa watoto- Rama Dee

Msanii wa muziki wa bongo fleva Rama Dee amefunguka na kusema kama angekuwa Rais wa Tanzania yeye angawekeza kwa watoto

kwani anaamini huwezi kuinyoosha bila ya kuangalia kizazi cha kesho akiamini kizazi cha sasa tayari kimesha athirika kwa msongo wa mawazo.

"Kwa mfano mimi nigekuwa Rais wa Tanzania, ningewekeza kwa watoto mana hauwezi kuinyoosha nchi bila kuangalia kizazi cha kesho, hiki chetu tayari kimeathirika, nchi ya Australia iligundua stress nyingi sana za wazazi zinaaribu maisha ya Watoto, hivyo walicho kifanya walitengeneza sheria ya mtoto, na kama mzazi ukipindisha unapelekwa mahakamani bila shaka. Waliweza kutengeneza mfumo wa "childcare" so hata kama mzazi hana kipato lakini serikali inaweza kusaidia mtoto akapata msingi mzuri wa kimaisha na kishule" alisema Rama Dee

Mbali na hilo Rama Dee anasema Child Care kwa nchi za wenzetu zinasaidia kuondoa utofauti wa mtoto wa mtu masikini na mtu tajiri kwani ukiwaweka pamoja wote wanakuwa sawa na kulingana kwa mambo mengi.

"Child care wanajaribu kusaidia wazazi wafanye kazi na mtoto apate malezi mazuri kupitia watu walio na uzoefu wa kulea watoto! ndio maana ukimsimamisha mtoto wa masikini wa mzungu na tajiri wote wapo sehemu sawa tu! hivyo dhumuni la serikali hapa ni kukamilisha au kutimiza ndoto za watoto" Rama Dee

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad