Njaa na Deni la Tiafa Kutikisa Bunge Kesho..!!!


Mkutano wa Sita wa Bunge unaanza Jumanne Januari 31, 2017 na kumalizika Februari 10, 2017 Mjini Dodoma, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano huo utaanza na kauli ya serikali kuhusu hali ya chakula pamoja na deni la taifa na hali ya uchumi nchini.

Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki.

Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:-

KIAPO CHA UAMINIFU
Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:-

    Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo
    Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi
    Mhe. Anne Kilango Malecela
    Mhe. Ali Juma Ali - (Jimbo la Dimani)

MASWALI

Katika Mkutano huu jumla ya maswali ya kawaida 125 yanatarajiwa kuulizwa na kujibiwa Bungeni. Aidha, kwa mujibu wa Kanuni ya 38 (1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge wastani wa maswali 16 ya papo kwa papo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu yataulizwa na kujibiwa pia siku za Alhamisi. 

KAULI ZA MAWAZIRI

Aidha, katika Mkutano huu wa Bunge Kauli mbili za Mawaziri zitawasilishwa  kama ifuatavyo:-
Kauli ya Serikali Kuhusu Hali ya Chakula Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.
Kauli ya Serikali kuhusu Deni la Taifa na Hali ya Uchumi Nchini itakayotolewa Tarehe 31 Januari, 2017.

MISWADA YA SHERIA

Katika mkutano huu, miswada ifuatayo itajadiliwa...

Muswada wa Sheria ya Sheria ya Madaktari wa Meno na Wataalam wa Afya Shirikishi wa mwaka, 2016 (The Medical, Dential and Allied Health Professionals Bill 2016).

Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016 (The Legal Aid Bill, 2016).

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali (Na.4) wa mwaka 2016. {The Written Laws (Miscellaneous Amendments)}, Bill, 2016) 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad