Awamu hii ya malipo ya faida ya utumiaji wa M-Pesa inafikia jumla ya Tsh Bilioni 32/- na itawawezesha watumiaji wa M-Pesa kuuanza mwaka vizuri ambapo kila mtumiaji atapata sehemu ya gawio kulingana na matumizi ya akaunti yake ya M-Pesa. Malipo haya yanafanyika kwa awamu na yatawanufaisha wateja na mawakala wa M-Pesa waliopo kila kona ya Tanzania. Ikiwa ni mwendelezo wa mtandao huo kuwarudishia faida ya gawio hilo kampuni hiyo imekwishagawa zaidi ya Tsh Bilioni 39 katika awamu zilizopita. Hii inamaanisha kwamba awamu hii itakapokamilika, ni zaidi ya Tsh Bilioni 70 zitakuwa zimewekwa moja kwa moja kwenye mifuko ya wateja wetu.
“Ugawaji huu wa faida ya kutumia M-Pesa kwa wateja na mawakala wetu ni muendelezo wa dhana kuu ya promosheni yetu ya”Nogesha Upendo”. Kila mtumiaji wa M-Pesa atapata pesa ya ziada kwenye akaunti yake, ambayo atakuwa na uhuru wa kuitumia vyovyote anavyopenda kama kununua vifurushi, kulipia huduma na bidhaa au kuwatumia ndugu na jamaa zake. Mteja mwenye matumizi makubwa kwenye M-Pesa, anapata gawio kubwa “zaidi la faida” Alisema Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.
Kuona kiasi cha gawio lako, tuma SMS yenye neno KIASI kwenda 15300. Utapokea SMS inayoonesha kiasi cha pesa kitakachotumwa kwenye akaunti yako. Vifurushi vya Cheka, Intaneti na YaKwakoTu vinaweza kununuliwa kwa kutumia gawio hili la faida. Kununua vifurushi kwa kutumia pesa uliyopokea, Piga *150*00# chagua NUNUA MUDA WA MAONGEZI/VIFURUSHI kisha chagua kifurushi unachohitaji.
Promosheni ya Nogesha Upendo ipo kwenye wiki ya 7 sasa ambapo zaidi ya wateja 200 washajishindia Tsh Milioni 1 pesa taslimu na 600 wengine wameshashinda Tsh 100,000/- za kila siku. Kuendelea kuongeza nafasi za kushinda zawadi za siku na wiki za hadi Tsh Milioni 1/- mteja anatakiwa kununua kifurushi chochote cha Vodacom ambapo ataingia kwenye droo moja kwa moja.