Omog: Ndiyo kwanza kazi imeanza

KOCHA wa Simba, Mcameroon, Joseph Omog ametamka kuwa wanaanza kutimiza ndoto zao na kuondoa nuksi ndani ya klabu hiyo ya kushindwa kupata mataji kwa kuanza na kuchukua ubingwa wa Kombe la Mapinduzi, leo Ijumaa watakapocheza dhidi ya Azam FC.

Omog anatarajiwa kuiongoza Simba katika fainali hiyo baada ya Jumanne ya wiki hii kuiondoa Yanga kwa penalti. Azam ambayo inanolewa na Idd Nassor Cheche kwa muda, yenyewe iliingia fainali hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar kwa kuifunga Taifa Jang’ombe katika nusu fainali. “Ile hali ya kukosa mataji kwa Simba itafika mwisho Ijumaa hii, tumejipanga vizuri kuchukua ubingwa, tunawaheshimu wapinzani wetu lakini kwa hali ilivyo inabidi

watusamehe kwani lengo letu ni moja tu la kutwaa ubingwa,” alisema Omog. Aidha, Kocha Msaidizi wa Simba, Jackson Mayanja naye alisema: “Tunajua Azam ina morali ya ushindi kwa kuwa waliwafunga Yanga mabao manne lakini sisi tuko vizuri na tayari kwa fainali.” Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa Azam, Cheche alisema: “Vijana wangu wote wapo vizuri, tunataka kupata matokeo mazuri zaidi ya tuliyoyapata tulipoifunga Yanga, hilo linawezekana kabisa, lakini ushindi ni ushindi. “Simba walitufunga kwenye ligi, lakini tuwaambie wasitegemee tena kutufunga kwa sababu mchezo wa fainali unakuwa na mipango yake.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad