Pesa Kupotea Mitaani… Machangudoa Watoa Kilio Chao kwa JPM



Dar es salaam:  Kufuatia hali ngumu ya kimaisha kutokana na pesa kutopatikana kirahisi kama ilivyokuwa awali, akinadada wanaofanya biashara haramu ya kuuza miili yao ‘machangudoa’ katika Jiji la Dar wametoa kilio chao kwa Rais John Magufuli ‘kulegeza’ kidogo kwani wanakufa njaa.

Machangu hao waliamua kufunguka hivyo hivi karibuni baada ya kuhojiwa na mapaparazi wa OFM waliokuwa wakifanya uchunguzi kuhusiana na biashara hiyo katika kipindi hiki ambacho kila mtu analia akisema ‘pesa imekauka mifukoni’.



Hali ikoje?

Katika utafiti huo uliofanyika katika maeneo ya Sinza Afrikasana, Kinondoni Makaburini na Buguruni jijini Dar, biashara hiyo imeonekana kudoda huku wengi wakieleza kuwa, hali hiyo imetokana na ugumu wa maisha.

Akizungumza na paparazi wetu, dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Pili, Mkazi wa Buguruni jijini Dar anayefanya biashara hiyo maeneo ya Sinza Mapambano alisema:

“Kiukweli hali ni mbaya sana, unajua wateja wetu wengi walikuwa wale ambao walikuwa wakipata pesa za kimagumushi, sasa baada ya Magufuli kubana, watu wamekuwa makini sana na pesa zao.

“Matokeo yake sasa, wateja wamekauka, unaweza kuja kijiweni, ukapigwa na baridi wee bila kupata mwanaume, ukarudi nyumbani mikono mitupu, kwa kweli hali ni mbaya.”

Naye Betty anayejiuza maeneo ya Sinza Mori jijini Dar alisema; “Kwa kweli itafika wakati inabidi tukalime, nimefanya biashara hii kwa muda mrefu lakini sijawahi kukumbana na ukata kama huu.

“Kuna miezi ambayo tunajua watu hawana pesa lakini kuna ile ambayo tunajua biashara itakuwa poa ila sasa hivi wateja hakuna mwanzo mwisho, yaani Magufuli ni noma, angelegeza kidogo.”

Hata hivyo asilimia kubwa ya machangu waliozungumza na OFM na kuulizwa kwa nini wang’ang’anie biashara hiyo hatarishi walisema, eti ndiyo ambayo imekuwa ikiwasaidia katika kuendesha maisha yao kwa muda mrefu.

“Wewe unadhani mimi nitakwenda kufanya nini, sijasoma wala sina ujuzi wowote, nimefanya biashara hii kwa muda mrefu, nimeichukulia kama ajira kwangu, sasa hali ikiwa mbaya hivi nikalie wapi? Watoto nitawasomesha na nini? Pango nitalipa na nini?” alisema dada mmoja aliyegoma kutaja jina lake.

Biashara kwa promosheni sasa

Katika maeneo ambayo OFM walitembelea, wasichana hao wakiwa wamevalia nguo za kihasara walionekana kugombea kila mteja aliyekatiza mbele yao na wakati mwingine kufikia hatua ya kupigana.

Aidha, tofauti na kipindi cha nyuma ambacho ukikutana na dadapoa anakupa bei ya kwenda kulala naye na ya ‘short time’, sasa hivi ni kwa promosheni na unaulizwa una shilingi ngapi, kiasi utakachotaja ni ngumu kukataliwa.

Wamepagawa

Kufuatia ukata huo, wadada wengi wanaofanya biashara hiyo wanaonekana kudata, ambapo wengi wamekuwa wakivuta bangi na kulewa sana kiasi kwamba ukikutana naye uso kwa uso, utaona dhahiri ni mtu aliyekata tamaa.

Wizi umeongezeka

Uchunguzi wetu umebaini kuwa, kutokana na wateja kupungua baadhi ya dadapoa hao wameanzisha tabia ya kuwaibia watu simu na pesa hasa katika maeneo ya Kinondoni na Buguruni.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad