Polepole Amtaja Anayeifitinisha Serikali


Katibu wa Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole amefunguka na kusema kuwa wanasiasa wa vyama vingine ambavyo siyo CCM wamekuwa na jihudi kubwa ya kuwachonganisha wananchi na kuwafitinisha na serikali.

Humphrey Polepole amesema hayo leo na kutoa wito kwa wananchi na kuwataka wawapuuze wanasiasa wanaotumia matatizo na majanga kuwa mtaji wao kisiasa kwani serikali ipo kwa ajili ya kuwahudumia.


"Wanasiasa wa vyama ambavyo si CCM wamekuwa na juhudi kubwa kufanya uchonganishi na kuifitinisha serikali na wananchi, tunatoa wito kwa wananchi kuwapuuza wanasiasa wanaotumia matatizo na majanga kuwa mtaji wao kisiasa, Serikali ipo ili kuwahudumia. Siasa yetu ni ya Ujamaa na Kujitegemea, tutaendelea kuhimiza Watanzania kujitegemea na kuongeza juhudi katika kazi" alisema Humphrey Polepole


Aidha amesema mageuzi makubwa yanayoendelea ndani ya CCM yanalenga kukiimairisha Chama kuisimamia Serikali na kushughulikia matatizo ya watu
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad