Q Chief Amwagia Sifa Mpenzi Wake ‘ni Wanawake Wachache Wenye Moyo wa Chuma Kama Wako’

Msanii wa muziki Q Chief ameshindwa kuzuia hisia zake mtandaoni na kuamua kumwagia misifa mpenzi wake.

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo Sungura, amedai mwanamke hiyo ni mwanamke wa pekee kutokana na uvumilivu wake.

“Soon tunatimiza miaka miwili katika uhusiano wetu umekuwa mvumilivu mwenye hekima ni wanawake wachache sana dunia hii wenye moyo wa chuma ulionao tumepita rough roads tumevuka vikwazo vingi tumepitia kila aina ya changamoto but most important tumepigana vita zote na kushinda sisi ni wababe wa vita love you honey, soon utatoka juani na utajikuta kivulini naamini maana Mungu wetu yu mwema nakizuri zaidi anatupenda sana,” aliandika Q Chief Instagram.

Muimbaji huyo ambaye ameweza kupambana na kuachana na matumizi ya Madawa ya kelevya, mapema mwaka 2016 alionekana akivalisha pete msichana huyo.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mwenye tabasamu kama hilo,akupende Umpende awe wako maishani.UTAMPATA WAPI KAMA HUYO .
    ULIKWISHA IMBA KAKA Q-CHILLA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad