Rais Magufuli: Serikali Yangu Haitayafumbia Macho Magazeti Mawili Yanayoandika Habari za Uchochezi

Rais John Magufuli amesema vyombo vya habari vinavyopotosha ukweli na kuleta uchochezi siku zake zinahesabiwa kwani Serikali yake anayoiongoza haiwezi kukubali kuvurugwa kwa amani ya nchi.

Amesema mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994 chanzo chake ni vyombo vya habari, hivyo hawezi kukubali hali hiyo itokee nchini.

Akizungumza kwenye uzinduzi wa Kiwanda cha Jambo Food Plant mjini Shinyanga na matangazo yake kurushwa mubashara na Star Tv, Rais Magufuli amesema magazeti yote isipokuwa mawili, vituo vyote vya televisheni na redio nchini vinafanya kazi nzuri ya kuelimisha wananchi.

Rais Magufuli amesema Serikali yake haikatai kukosolewa na kwamba, magazeti mengine yanakosoa na kusaidia kutatua matatizo ya jamii, lakini hayo mawili (bila kuyataja) yamekuwa ni kupindisha kila kitu.

“Hayo magazeti kila ukisema hivi yanapindisha, siyataji kwa sababu yanajifahamu lakini yajue kwamba siku zake zinahesabika. Serikali ninayoiongoza haiwezi kukubali amani kuvurugwa,” amesema.

Chanzo: Mwananchi

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nape ameshakusikia Mkuu
    Atafungia karibuni, wewe si umeuziwa hii Nchi ufanye unavyotaka???

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sikio liliponza kichwa ndugu kuwa makini na maneno yako

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad