Wakati Rais wa Uturuki, Recep Erdogan akitua nchini leo, uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania umesaidia kukua kwa biashara kutoka Dola66 milioni za Marekani (zaidi ya Sh 135 bilioni) hadi Dola180 milioni (zaidi ya Sh360 bilioni).
Taarifa iliyotolewa jana na Katibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mustafa Efe Uzman ilisema kushamiri huko kuliongezeka zaidi katika kipindi cha mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, Uzman alieleza kuwa Uturuki inaamini uhusiano huo utainua hadhi ya Watanzania ambao nchi yao ni miongoni mwa mataifa yanayokua kiuchumi katika Afrika Mashariki.
“Sehemu ya uhusiano wa kiuchumi kwa pande hizi inajumuisha safari za ndege za moja kwa moja za kutoka Istanbul hadi Dar es Salaam,” alisema katibu huyo.