Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Ujasusi la Marekani (CIA), John Brennan amemuonya Rais Mteule wa
Marekani, Donald Trump kuwa makini na kauli zake na kuuchunga mdomo
wake, hasa anapozungumzia suala la uhusiano wa kidiplomasia kati ya
Marekani na Urusi kwa madai kwamba anahatarisha usalama wa Taifa la
Marekani.
Brennan aliendelea kueleza kuwa, Trump
bado hajaelewa nia ya Urusi kwa Marekani kwa hiyo badala ya kufurahia
mipango ya siri inayoendelea, anapaswa kuwa makini na kuchunga kauli
zake.
“Nafikiri Trump haelewi kwa sababu gani
uhusiano wa Marekani na Urusi umekuwa suala tete kwa kipindi kirefu
kilichopita, anatakiwa kuwa makini sana anapolishughulikia suala hili,”
alisema na kuongeza kuwa CIA inazo taarifa za namna Urusi inavyojaribu
kumtumia Trump kutimiza matakwa yake.
John Brennan
Brennan aliyazungumza hayo wakati
akihojiwa na Kituo cha Runinga cha Fox News, ikiwa ni wiki moja tangu
alipotangaza ripoti kwamba wamegundua kuwa Rais wa Urusi, Vladimir Putin
na vijana wake, walifanya ‘makeke’ ili Trump ashinde kwenye uchaguzi
mkuu nchini humo, na kumuangusha kwa hila mpinzani wake, Hillary
Clinton.