Mji wa Bula Hawa nchini Somalia umepiga marufuku harusi za gharama ya juu ili kuwashawishi vijana wengi zaidi kuoa.
Kamishna wa Mji wa Bula Hawa uliyo
karibu na mpaka wa Kenya, Mohamud Hayd Osman amesema kwamba, mbuzi
wasiozidi watatu ndio wanaofaa kuchinjwa pekee ili kuwalisha wageni na
kwamba sherehe katika hoteli hazitaruhusiwa.
Amesema kuwa mahari itakuwa chini ya
dola 150 (sawa na TZS 350,000/=) pekee ambapo uamuzi huo umekuja baada
ya maafisa kubaini kwamba takriban watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa
hivi karibuni
Kamishna huyo ameongezea kwamba gharama
ya harusi, ukosefu wa ajira na kiangazi ndio maswala yanayowafanya watu
kulihama eneo hilo.
Waandishi wanasema sio kawaida kwa familia ya bwana harusi kutumia takriban dola 5000 katika harusi nchini Somalia.
“Mafunzo ya kiislamu yanasema kuwa ndoa inafaa kuwa ya gharama ya chini,” alisema Osman.
Hatua ya kupunguza matumizi kuhusu
sherehe za kifahari pamoja na matumizi mengine baada ya ya maafisa
kugundua kwamba ni kwa nini watoto 150 walizaliwa nje ya ndoa mjini
humo. Wasichana walikuwa wanakataa kuolewa hadi pale kitita cha pesa
kitakapotumika kwa dhahabu pamoja na fanicha, alisema.