Ray Aaamua Kumwanika Mtoto Wake wa Kiume Hadharani,Adai Weupe Wake Hautokani na Kunywa Maji..!!


Ray alipost picha kuonyesha sehemu ya mwili ya mtoto wake

Mpenzi wa msanii mkongwe wa filamu Ray Kigosi, Chuchu Hans amejifungua mtoto wa kiume wiki hii, Ray amethibitisha.


Muigizaji huyo ameonyesha furaha yake kwa kuwa huyo ni mtoto wake wa kwanza.


“Asante mungu kwa kuniletea pacha wangu asante my lovely mzungu kwa kunipa heshima kubwa kunifanya niitwe baba, mungu wangu wa haki asiyeshindwa na jambo akubariki sana,” muigizaji huyo aliandika Instagram.

Aliongeza, “Sasa msianze maneno yenu kwamba mwanangu amekunnywa maji, mtoto bado ni mchanga maana watu wa Insta kiboko lakini hawaishi mtoni,”

Kwa upande wa Chuchu Hans huyo ni mtoto wake wa pili, mtoto wake wa kwanza alizaa na mume wake wa zamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad