Ripoti yasema Wanawake wa Ulaya wanapata watoto wachache

 Matukio mengi ya kiuchumi na kitamaduni katika kipindi cha nusu karne iliyopita vinaonekana kusababisha wanawake na wanaume kuepuka kupata watoto

Wanawake barani Ulaya wanapata watoto wachache, hususan kusini mwa bara hilo, ripoti ya Ufaransa imebaini.

Zaidi ya asilimia 5% ya wanawake waliozaliwa miaka ya 1970 huenda wakabakia kutokuwa na watoto kusini mwa Ulaya , ikilinganishwa na asilimia 15% katika mataifa ya kaskazini mwa Ulaya na asilimia 18% katika nchi za magharibi mwa Ulaya.

Sababu zinazochangia ni ukosefu wa soko la ajira na ukosefu wa sera bora za kazi zinazozingatia maisha ya kifamilia, jambo linalosababisha kuongezeka kwa idadi ya watu wanaojitolea kutokuwa na watoto, imeelezea ripoti hiyo.

Lakini ripoti imeelezea kwamba viwango vya watu wasio kuwa na watoto pia vilikuwa vya juu yapata karne moja iliyopita.
 Upungufu wa watoto unaonekana zaidi kusini mwa bara Ulaya

Kiasi cha asilimia 17 hadi 25% ya wanawake waliozaliwa katika karne ya 20 walibakia kutokuwa na watoto, kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo vifo vya wanaume wengi wa umri wa kuoa kufa katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, uhamiaji wa vijana wa kiume katika nchi maskini, na athari za mfadhaiko mkubwa wa mwaka 1929.

Tangu wakati huo kulikuwa na idadi kubwa ya watu wasiokuwa na watoto, inasema Taasisi ya masuala ya Idadi ya watu nchini Ufaransa.
Mashariki mwa Ulaya , ongezeko kubwa la idadi ya watoto wanaozaliwa lilidumu zaidi kuliko magharibi

Upungufu wa watoto ulifikia viwango vya chini zaidi miongoni mwa wanawake waliozaliwa kati ya miaka ya 1930 na 1940 - wazazi wa kizazi cha "baby boom" ambacho kiliishi na kunufaika na mafanikio ya baada ya vita kama vile viwango vya chini vya ukosefu wa ajira na hali ya mifumo bora ya kijamii iliyotolewa na serikali za wakati huo.

"Matukio mengi ya kiuchumi na kitamaduni katika kipindi cha nusu karne iliyopita vinaonekana kusababisha wanawake na wanaume kuepuka kupata watoto.

Wanawake wachache imeeleza ripoti kuhusu kupungua kwa watoto barani Ulaya , kutokuwa na mpango wa kupata watoto - badala yake , wengi wao "wamekuwa wakiahirisha uzazi" hadi kujipata mud..

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad