Serikali Yanunua Shule ya CCM

Hatimaye Rais John Magufuli amehitimisha mjadala wa matumizi ya fedha za msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera kwa kukarabati Shule ya Sekondari ya Omumwani inayomilikiwa na CCM kisha Serikali kuinunua.

Novemba mwaka jana, Meya wa Manispaa ya Bukoba, Adronicus Karumuna alilalamikia zaidi ya Sh70 milioni za tetemeko hilo lililotokea Septemba 10 mwaka jana na  kusababisha vifo vya watu 17 na kuharibu miundombinu mbalimbali, kutumika kukarabati shule hiyo ya Jumuiya ya Wazazi huku waathirika wakiwa hawajapata msaada wa maana.

Shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 1966 ikiwa ya kwanza ya Wazazi nchini, ilikarabatiwa na Serikali ili kuiwezesha kupokea wanafunzi wa Sekondari ya Ihungo baada ya shule yao kuharibika kwa tetemeko.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad