Serikali Yatoa Tamko Hili Juu ya Uwepo wa Ugonjwa wa Mafua ya Ndege..!!!


SERIKALI imesema hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa wa mafua ya ndege nchini.


Akizungumza  katika mahojiano maalumu  jana, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hakuna mgonjwa yeyote aliyepatikana na ugonjwa huo nchini hadi sasa.

Ummy alisema hayo akitoa ufafanuzi baada ya kuenea uvumi kwamba kisiwani Zanzibar, amepatikana mgonjwa mwenye mafua ya ndege.

Alisema kutokana na kuibuka kwa ugonjwa huo nchi jirani serikali imetuma watalaamu mpakani mwa Tanzania na Uganda kutoa elimu kwa wananchi namna ya kujihadhari na ugonjwa huo.

Aliwataka madaktari wote nchini wakimwona mgonjwa mwenye dalili au mafua yasiyo ya kawaida, kumpima na kumpa tiba haraka kabla hajaugua au hajaambukiza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad