SMG, risasi 30 vyaokotwa kichakani

Kibaha. Silaha ya kivita aina ya SMG na risasi 30 mali ya Hifadhi ya Taifa ya Saadani vimekutwa vimefichwa kwenye kichaka jirani na Mto Kitame katika Kata ya Makurunge wilayani Bagamoyo mkoani Pwani.

Silaha hiyo inadaiwa iliibwa kwenye Geti la Gama saa tisa usiku Desemba 24, mwaka jana wakati askari wa hifadhi hiyo, Jackson Shirima (23) akiwa kazini.

Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bonaventura Mushongi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya askari huyo kutoka lindo getini hapo na kujipumzisha kwenye moja ya mahema akiwa na silaha hiyo.

“Askari huyu alikuwa zamu na kama ilivyo ada huwa wanapokezana, hivyo alitoka na silaha akaenda kujipumzisha kwenye hema maana hifadhini hutumia mahema na alipitiwa na usingizi ndipo ilipoibwa na mtuhumiwa aliyewahi kuwa mtumishi wa hifadhi,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad