Wabunge na mawaziri
wametii agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai lililowataka kuzingatia
mahudhurio ya vikao vya kamati za Bunge, vinginevyo majina yao
yangewasilishwa kwa mamlaka wanazowajibika ikiwamo kwa Rais John
Magufuli.
Katika
mkutano wa nne wa Bunge mwaka jana, Spika Ndugai alisikitishwa na
mahudhurio hafifu ya mawaziri na wabunge katika vikao vya kamati
vilivyofanyika kuanzia Septemba 22 hadi Oktoba 2 mjini Dodoma.
Amesema
katika vikao hivyo vya kamati ilitengenezwa orodha ya wabunge na
mawaziri watoro, ambayo ataitunza hadi vikao vingine vya kamati.
Spika
Ndugai aliwaonya kuwa iwapo wataendelea na tabia ya utoro kwa vikao
vya kamati vilivyofanyika kati ya Oktoba 17, 2016 angewashtaki kwa
wapigakura, vyama vyao na mawaziri angewafikisha kwa Rais Magufuli.