Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limeeleza kiini cha tatizo la kukatika umeme nchi nzima kwa siku ya leo pamoja na jitihada ambazo limezifanya ili kurejesha hali ya kawaida katika mikoa iliyo kwenye gridi ya taifa
Meneja wa Mifumo wa TANESCO Mhandisi Abubakar Hisa amesema, Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza umeme chenye uwezo wa kuzalisha KV 32 kimepasuka na kudondoka na kwamba wataalamu wamepelekwa mkoani Tanga kwa ajili ya marekebisho.
Aidha, Mhandisi Hisa, ameongeza kuwa hadi kufikia tarehe 27 majira ya usiku mafundi wa TANESCO watakuwa wamekamilisha matengenezo ya kituo hicho na kupelekea hali za usambazaji umeme kwa nchi nzima kurejea katika hali yake ya kawaida.
Shirika hilo limesema kuwa mafundi wake wanaendelea na jitihada za kurejesha umeme katika hali yake ya kawaida baada hii leo kutokea kwa hitilafu katika kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza umeme cha Ubungo na kupelekea Mikoa kadhaa kukosa umeme kwa zaidi ya muda wa saa 5.
Kufuatia jitihada zinazofanywa na mafundi wa TANESCO kuanzia majira ya saa kumi na mbili na nusu alfajiri ya leo hadi kufikia majira ya saa 7 mchana baadhi ya mikoa iliyounganishwa kwenye Gridi ya Taifa ilianza kupata umeme japo kwa maeneo kadhaa ambayo hayauwekwa wazi.