TFF Imemteua Huyu Hapa Kuwa Kocha wa Taifa Stars


TFF imemteua Salum Mayanga kuwa kocha wa muda, wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kuchukua nafasi ya Kocha Charles Boniface Mkwasa ambaye mkataba wake unafikia mwisho mwezi Machi, mwaka huu - 2017.

Kati ya majukumu yake yatakuwa ni kuandaa kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 ambazo mechi za awali zitanza mapema mwaka huu.

Pia Kocha Mayanga atakuwa na jukumu la kuandaa kikosi cha wachezaji wa ndani kwa ajili ya hatua ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN).
TFF inamshukuru Kocha Charles Boniface Mkwasa kwa utumishi katika nafasi hiyo ulioanza Julai, 2015 na kumtakia mafanikio katika mipango yake inayofuata.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tutaona na wewe utafikia wapi. Hawa makocha ni watu wa kuwapatia mikataba mifupi mifupi tu. Mkataba wa miezi mitatu unatosha kabisa. Ili hata akivurunda lile Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania linakuwa halibanwi sana na mkataba baina yao na huyo kocha. Kwanza ni kwa nini hiyo mikataba na hawa makocha isiwe wazi kiasi cha kumfanya huyo kocha kuwajibika na ikiwezekana atumbuliwe mara moja pale Timu ya Taifa inapovurunda katika mechi yao ya kwanza.

    ReplyDelete
  2. Hii mikataba ya muda mrefu ya hawa makocha uchwara ndio yanaifanya Timu ya Taifa ionekane kichwa cha mwenda wazimu kila kukicha.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad