Katika kipindi cha miezi sita ya
mwaka wa Fedha 2016/17 yaani kuanzia Julai hadi Disemba 2016, Mamlaka ya
Mapato Tanzania (TRA) imekusanya kodi jumla ya shilingi trilioni 7.27
ikilinganishwa na shilingi trilioni 6.44 ambazo zilikusanywa kipindi
kama hicho mwaka wa fedha 2015/16.
Ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha 2016/17 umeongezeka kwa asilimia 12.74.
Mlinganisho wa makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2015/16 na 2016/17 ni kama ifuatavyo:
MWEZI | MWAKA 2015/16 | MWAKA 2016/17 | Ongezeko |
JULAI | 925,384.7 | 1,069,458.5 | 15.57 |
AGOSTI | 923,316.9 | 1,154.222.5 | 25.01 |
SEPTEMBA | 1,132,310.3 | 1,378,048.9 | 21.70 |
OKTOBA | 1,037,179.8 | 1,131,094.9 | 9.05 |
NOVEMBA | 1,027, 939.6 | 1,123,509.7 | 9.30 |
DISEMBA | 1,403, 189.8 | 1,414,921.8 | 0.84 |
JUMLA | 6,449,321.1 | 7,271,256.26 | 12.74 |
Jitihada mbalimbali zinafanywa
ili kuhakikisha TRA inaongeza makusanyo kwa kuongeza ufanisi katika
ukusanyaji, kuhimiza maadili mema kwa watumishi, kuboresha mifumo ya
ukusanyaji, kushirikiana na vyombo vingine vya dola na wananchi katika
kuziba mianya ya upotevu wa mapato pamoja na kufuatili, kuhimiza
matumizi ya mashine za kielektronik na kuhimiza ulipaji wa kodi ya
majengo.
TRA inaendelea kuhimiza
wafanyabiashara wote waliosajiliwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
kuwasilisha ritani za VAT kabla ya tarehe 20 ya kila mwezi kama
ilivyobadilishwa katika Sheria ya Fedha ya 2016.
Pamoja na hayo tunawakumbusha na
kuwahimiza wananchi wa Dar es Salaam ambao hawajafanya uhakiki wa
taarifa za Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kuhakiki taarifa zao
kabla ya tarehe 31 Januari 2017 ili zoezi hilo liweze kuanzishwa katika
mikoa mingine.
TRA inatoa wito kwa
wafanyabiashara kulipa kodi stahiki kwa hiari na wakati ili serikali
ipate mapato yake ambayo yataiwezesha kuwahudumia wananchi wake
kikamilifu.
Kwa wafanyabiashara wenye madeni
ya nyuma wanashauriwa kujitokeza kuonana na Mameneja wa Mikoa na Wilaya
kujadiliana jinsi watakavyolipa madeni yao bila kuathiri biashara zao.
Wamiliki wa majengo wanaaswa kutoa ushirikiano kwa kulipia ankara zao za kodi ya majengo kwa hiari .
‘Pamoja Tunajenga Taifa Letu’
Richard M. Kayombo
MKURUGENZI WA HUDUMA NA ELIMU KWA MLIPAKODI