Trump Like Magufuli Bana, Naye Kaanza Kutumbua Majipu, Aawafuta Kazi Mabalozi Wote wa Marekani Duniani


Kwa mujibu wa  The Independent na ParsToday wanasema kuwa Rais Donald Trump wa Marekani amewafuta kazi mabalozi wote wa nchi hiyo kote duniani na wanaohudumu katika mashirika ya kimataifa ambapo uamuzi huo umefanyika katika siku yake ya kwanza kazini.

Trump ambaye aliapishwa Ijumaa January 20, 2017 kuwa Rais wa 45 wa Marekani, amewataka mabalozi wote walioteuliwa na mtangulizi wake, Barack Obama kuondoka kazini mara moja bila hata kuwapa muda wa kujitayarisha kuondoka kama ilivyo kawaida.

Inaelezwa kuwa zaidi ya mabalozi 80 wa Marekani katika nchi mbalimbali duniani walifutwa kazi Ijumaa tarehe 20 Disemba saa sita mchana ikiwa ni mara baada ya Trump kuapishwa.

Hatua hiyo ya Trump inatazamiwa kuvuruga uhusiano na washirika muhimu kama vile Ujerumani, Uingereza na Canada ambapo ripoti zinasema nchi hizo zinaweza kukaa bila mabalozi kwa miezi kadhaa kwani baada ya Trump kuteua mabalozi wapya watalazimika kuidhinishwa na Bunge la Congress kabla ya kuanza kazi zao.

Donald Trump anakosolewa kwa kuacha nafasi nyingi wazi na hivyo kuvuruga shughuli za kawaida za serikali ya Marekani na hii haya yanajiri huku maandamano yakiripotiwa kuendelea sehemu mbalimbali kupinga utawala wa kiongozi huyo.

Nchini Marekani katika siku ya pili ya utawala wa Trump kumeripotiwa maandamano ya watu milioni tatu na imeripotiwa kumefanyika maandamano 637 katika maeneo mbalimbali ya Ulaya, Asia na Afrika kumpinga rais mpya wa Marekani.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hazilingani hizi mbili. Kama mnakosa ya maana kuandika semeni.

    ReplyDelete
  2. Magu is a Game changer in African Leadership. Huyu si kiongozi wa Tanzania Tu. Ni kiongozi wa Kimataifa. Mwenye Vision and Mission. JPJM austerity measure alizozichukua is second to Non. Wanaomfata nyao za uongozi wake ni wengi akiwemo NAMO ( Narendra Modi).. na wengine wengi na sasa new onboard ni Tramp. Nacheza na Magu. Orijino Tanzania. Hapa Kazi Tu. JPJM Tunakuamini na imedhihirika katika uchaguzi mdogo wa majuzi.. CCM inakubalika kiakili na Moyoni. mpaka huko 2025 uwanja ni Wako JPJM. na tunazidi kukuombe Mungu akupe Afya na Akulinde Ututumikie.

    ReplyDelete
  3. Magu is a Game changer in African Leadership. Huyu si kiongozi wa Tanzania Tu. Ni kiongozi wa Kimataifa. Mwenye Vision and Mission. JPJM austerity measure alizozichukua is second to Non. Wanaomfata nyao za uongozi wake ni wengi akiwemo NAMO ( Narendra Modi).. na wengine wengi na sasa new onboard ni Tramp. Nacheza na Magu. Orijino Tanzania. Hapa Kazi Tu. JPJM Tunakuamini na imedhihirika katika uchaguzi mdogo wa majuzi.. CCM inakubalika kiakili na Moyoni. mpaka huko 2025 uwanja ni Wako JPJM. na tunazidi kukuombe Mungu akupe Afya na Akulinde Ututumikie.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad