TUHESHIMU tu Wataalam na Wanataaluma-Habib Mchange


iki hii nimekumbuka namna Dr. Idrissa Rashid mwaka 2008 alipoishauri Tanesco kiuchumi iinunue mitambo ya Dowans tena kipindi hicho ilikuwa inauzwa bei ya 'kutupwa'.

Wachumi wenzake kina Zitto Kabwe wakamuunga mkono tuinunue itatusaidia huko mbeleni.

Wanasiasa wakapinga kwa kelele nyingi, wakasema mitambo mibovu, chakavu haifai na wakaenda mbali wakasema Kina Zitto wanatetea kisa wamehongwa na Kina Rostam.

Wakaongeza kuwa sheria ya manunuzi ya mwaka 2004 inatukataza kununua vitu vya mtumba

Waliosema haya Leo wengine ni mawaziri waandamizi wa serikali ya JPM na wengine ni viongozi na wabunge machachari wa UPINZANI.

Wanasiasa wakashinda. Mitambo tukaiachia, na kesi tukashindwa, tukalipa zaidi ya Bilioni 90 kwa kosa la kuvunja mkataba bila kufuata utaratibu. .

Mitambo Ile Ile mibovu, chakavu na ya kifisadi.

Marekani wakainunua, ikabadilishwa Jina ikaitwa Symbion.

Ikaanza kuzalisha umeme na kuiuzia Tanesco.

Obama akaja kutoka Marekani akaizindua.

Wale wale Waliosema mibovu wakaisifia na kuipongeza Marekani.

Mitambo ambayo tungeinunua tungeimiliki wenyewe wala tusingeuziwa umeme.

Leo tunauziwa umeme ghali kutokana na mitambo tuliyoruhusu wanasiasa wawapuuze wataalam.

Hivi ninavyoandika Symbion wanatuuzia umeme kutoka kwenye mitambo ya mtumba.

Sheria inatukataza kununua mitambo ya mtumba lakini inaturuhusu kununua umeme unaotokana na mitambo ya mtumba.

Tuwaheshimu wataalam wetu.
Habib Mchange
Mwananchi
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. VIONGOZI WATANZANIA NI WEZI , KAZI WAO NI KUWAIBIA MASKINI NA KUJINUFAISHA WANYE.... VIVA MAGUFULI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad