TUNDA la Tikitimaji Lina Faida Nyingi Mwilini na Hutibu Baadhi ya Maradhi...

Tunda la tikitimaji au kwa Kiingereza Watermelons lina faida nyingi mwilini na hutibu baadhi ya maradhi.

Tikitimaji pia ni chanzo kikuu cha protini, mafuta, nyuzinyuzi, wanga, calcium, phosphorus, chuma,vitamin A, B6, C. potasium, magnesium, carotene, anthocyanins na virutubisho vingine vingi katika mwili.

Tunda hili linasaidia mtu kuwa na uwezo mkubwa wa kuimarisha misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa hatari ya kupata shinikizo la damu.

Tiba au faida 13 za tikitimaji kiafya ni nyingi, asilimia 92 ya tunda hili ni maji, hivyo mtu akila anaongeza maji mwilini, lina vitamini A ndani yake, huboresha afya ya macho, kuna vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili, husaidia kuponya majeraha, hukinga uharibifu wa seli na huboresha afya ya meno na fizi.

Faida nyingine ya tunda hili ni kwamba lina vitamini B6 ambayo  husaidia ubongo kufanya kazi vema, hubadilisha protini kuwa nishati na ni chanzo cha madini ya potasiamu pia husaidia kushusha na kuponya  shinikizo la damu, hurahisisha mtiririko wa damu mwilini, huondoa sumu mwilini, huongeza nguvu za kiume hasa ukila pamoja na mbegu zake.



Usikose kula tunda hili kila wiki utaona faida yake.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ni kweli ili tunda ni la kipekee,nimejionea mwenyewe linavyoimarisha afya yangu,mwenyezi mungu apewe sifa kwa uuambaji wake.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad