UFAFANUZI wa Zitto Baada ya Baadhi ya Wabunge Kutofurahishwa na Tamko lake


December 30 2016 mbunge wa kigoma mjini na kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe alitoa taarifa kuhusu madeni anayodaiwa, kiwango cha mshahara wake wa mwaka, kiasi cha pesa kilichopo benki, posho pamoja na mali zote anazomiliki.

Kupitia ukurasa wake wa facebook ametoa ufafanuzi akidai baadhi ya wabunge wenzake hawajafurahishwa namna alivyoweka na hivyo ameeleza kuwa….

Mshahara wa mbunge kwa mwezi ni tshs 4.6 milioni kabla ya kodi, baada ya kukatwa kodi ya mapato mbunge hubakia na tshs 3.2 milioni kwa mwezi. Hivyo Mshahara ni tshs 38.4 milioni kwa mwaka.

Mbunge hulipwa pia tshs 8.2 milioni kila mwezi kama posho ya kazi za Ubunge (mafuta ya kutembelea Jimbo, matengenezo ya gari, malipo ya watumishi wa Ofisi ya Mbunge kama vile Dereva, mhudumu wa ofisi na Katibu wa Mbunge). Hii ndio inapelekea mapato ya jumla ya tshs 99 milioni kwa mwaka niliyoweka kwenye taarifa ya rasilimali na madeni.

Mbunge pia hulipwa posho za kujikimu na posho za vikao ( kwa wale wanaochukua posho hizi). Hizi hutolewa kulingana na mahudhurio ya vikao.

Aidha zitto ameongeza kuwa kuweka wazi tamko la mali na madeni kwa sasa sio takwa la kisheria bali ni uamuzi binafsi wa Mbunge ama Kiongozi mwengine wa umma.

Mimi ninatakiwa na katiba ya chama changu kuweka wazi tamko la mali na madeni kwa mujibu wa azimio la Tabora linalohuisha azimio la Arusha. Hivyo, ichukuliwe kuwa kuweka kwangu wazi tamko husika ni kutekeleza matakwa ya katiba ya chama ambacho Mimi ni mwanachama na sio kuwashtaki wenzangu kwa wananchi. Mimi naamini kwamba uwazi ni moja ya silaha madhubuti ya kupambana na ufisadi. Nimewasilisha muswada bungeni kutaka uwazi huu liwe sharti la sheria za nchi yetu;-Zitto
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Well said young man , giving you a pat on your shoulder.

    ReplyDelete
  2. Kumbe Ubunge Ni Dili...Haiwezekani. Sisi Watanzania wenye Nia ya kuijenga nchi yetu na kuitumikia tulipwe hivi na wenzetu hata dawa na usafiri hawana

    ReplyDelete
  3. Wala msiwe na wasi wasi Majaliqa yupo na Magu kashika hatamu. hili suala wanalielewa na mikakati iko njiani. na hawa wasiojiheshimu waheshimiwa na watoro ndiyo wafaidikaji wakuu. haya malipo wali idhinishwa wakati wa miundo mbinu hewa na watekelezaji Hewa katika shamba la bibi. tutaanzisha referendum within to have the mind set. with an action plan...HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  4. Wala msiwe na wasi wasi Majaliqa yupo na Magu kashika hatamu. hili suala wanalielewa na mikakati iko njiani. na hawa wasiojiheshimu waheshimiwa na watoro ndiyo wafaidikaji wakuu. haya malipo wali idhinishwa wakati wa miundo mbinu hewa na watekelezaji Hewa katika shamba la bibi. tutaanzisha referendum within to have the mind set. with an action plan...HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  5. Kabwe mbona unaamua kututosa na pia utazama!! na ya NSSF pia wewe ndani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad