Waziri Mkuu Mstaafu na Mgombea wa
Urais 2015 kupitia CHADEMA, Edward Lowassa leo alikamatwa na jeshi la
Polisi wakati akiwa anaenda kwenye kampeni za uchaguzi Kata ya Nkome na
baadaye aliachiwa huru ambapo taarifa za polisi zinadai kuwa walimzuia
kwa sababu za kiusalama.
Kupitia kituo cha Television cha Azam
wameripoti habari ya kukamtwa kwa Lowassa ambapo baadhi wa wananchi
wameeleza tukio lilivyotokea.
“Tulikuwa kwenye msafara ya
kumpokea Lowassa lakini tulipofika hapa stendi wananchi walitaka kuongea
na Lowassa, kabla hata hajashuka kwenye gari askari walituvamia
wakasema tuondoke moja kwa moja twende kituoni”– shuhuda.
Mbali na hivyo, Polisi walilazimika
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wanaoandamana kwenda
kituo cha polisi baada ya Lowassa kukamatwa.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita
amesema kuwa hawakuwa wamemkamata Edward Lowassa bali walikuwa
wakijadiliana naye kuhusu usalama wake na jamii.