Ilidaiwa kwamba sababu ya gari hilo kukamatwa ni kosa la kutokuwa na vibali halali huku Polisi ikimtaka Zitto ajitokeze.
Mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Mama Anna Mugwhira ameongea na AzamTV kuhusu uwepo wa taarifa za kutoonekana kwa kiongozi wa ACT Zitto Kabwe.
‘Zitto alikuwa anatafutwa na polisi na mimi nilikuja kusikia gari limekamatwa lakini yeye aonekani, inaonekana yeye aliposhuka aliondoka na njia nyingine tofauti hakuondoka na gari lake, sisi kama chama hatukufikia mahali pa kufikiri kwamba hayupo au haonekani na taarifa zilizokuwa zinapatikana zilisema yupo Kahama, taarifa rasmi haijatolewa na yeye mwenyewe’;-Anna Mugwhira
Tazama Video:
Inawezekana vipi wewe Kiongozi Mzima wa Chama hujui Kiongozi mwenzako alipo na wala hujawasiliana naye mpaka upate taarifa kupitia vyombo vya habari. Nadhani huo ni uongo na uzembe wa hali ya juu miongoni mwa nyie viongozi wa upinzani. Hamna uwajibikaji wa pamoja na hiyo inatutia wasiwasi sisi Wananchi wa kawaida. Sasa leo ndio kama mnaonyesha hali ya aina hiyo hata kabla hamjakamata Nchi, je kesho na keshokutwa mkikamata Nchi ndio itakuwaje??? Kwa kweli nyie ni watu wa hovyo sana na ndio maana hatuwezi kuwapigia kura.
ReplyDeleteEeeeeh!hii kali,Mama unatuangusha.
ReplyDeleteCHAMA KINAKUFA.