Zanzibar. Vigogo wawili wa siasa za upinzani nchini, Edward Lowassa na Maalim Seif Sharif Hamad jana walitumia fursa ya kumnadi mgombea ubunge Jimbo la Dimani kwa tiketi ya CUF, Abdulrazaq Khatib Ramadhan kulalamikia utawala uliopo madarakani kuwa unaendesha mambo kibabe.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Lowassa ambaye pia ni Waziri Mkuu wa zamani na Maalim Seif aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar katika Serikali iliyopita, waligombea urais wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, mtawalia.
Maalim Seif alia na JK
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za mgombea huyo kwenye Skuli ya Fuoni, Zanzibar, Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu CUF, alisema chanzo cha mgogoro wa Zanzibar kuhusu Uchaguzi Mkuu uliopita ni Rais mstaafu, Jakaya Kikwete.
Alidai kwamba Kikwete ndiye aliyefifisha matakwa ya Wazanzibari walio wengi ya yeye kuwa Rais wao.
Alisema kazi kubwa ilikuwa imekamilika ya kuhakikisha Wazanzibari wanakuwa na Rais wamtakaye.
Sijui watu tumechoka siasa ama vipi maana nilitegemea kwa ujio wa Muheshimiwa Lowasa watu tungekuwa hapatosha.
ReplyDeleteMimi mwenyewe nilishangaaa.
Delete