Viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), wamelalamikia kuchezewa rafu katika uchaguzi mdogo wa ubunge na madiwani baada ya CCM kuibuka na ushindi, wakiachia kata moja tu.
Lakini, CCM Zanzibar imesema ushindi ilioupata Jimbo la Dimani ni ishara kwamba Watanzania bado wanaendelea kukiamini chama hicho na kukipa dhamana ya kuwaongoza.
Juma Ali Juma aliiwezesha CCM kutetea kiti chake cha ubunge wa Dimani, jimbo pekee lililorudia uchaguzi baada ya kuachwa wazi na Hafidh Ali Tahir aliyefariki dunia Novemba mwaka jana akiwa bungeni mjini Dodoma.
CCM pia imeibuka mshindi katika kata 18 kati ya 19 za Tanzania Bara.
ccm mbele kwa mbele
ReplyDeleteVuteni kamba ili mfike. Msisahau vijijini. Ingawa mna misukosuko. Hii ni ,itihani. Inabidi wote unganeni. Wote wapinzani inabidi muungane sasa kwa kutetea maslahi ya nchi hii. Wekeni tofauti zenu kando. Dalili nyingi zinajionyesha wazi. Utawala wa sasa muelekeo kamili haujulikani.Tunawaita wawekezaji tunaponda elimu kwa Wananchi na watoto. Uwekezaji kwa kipindi hiki ilobidi ni kwa Watanzania wajiwekezee wenyewe. Uturuki na rushwa kwao, hashishi, nadawa ya kulevya. Meli zilizoandikishwa kutumia jina Tanzania. Maslahi yao chuma chomoa ondoka. Nani asiyejua hili?
ReplyDeleteUmaskini wa kufikiri ni chanzo cha uongozi na maendeleo kwa Wananchi.