Wanachama 200 Waikimbia CHADEMA na Kujiunga CCM

Chama   cha  Demokrasia  na Maendeleo (Chadema), kimeendelea  kupata  pigo  baada  ya  wanachama  200, wakiwamo  viongozi  wa Kitongoji  cha Kwemghogho Mahezangulu kujitoa  na  kujiunga  na  Chama Cha Mapinduzi (CCM) .

Akizungumza  baaada ya  kupokea  wanachama  hao, Mbunge wa  Bumbuli, January Makamba (CCM),  alisema  wananchama  hao  wameamua  kurudi  wenyewe nyumbani   kutokana  na   kuona  ahadi  nyingi  za maendeleo zimetekelezwa  kwa  kiasi kikubwa.

Alisema  chama  chake kimefanya mambo mengi  hivyo  haoni  ajabu  ya  kupokea  wanachama kutoka  vyama  vingine  vya  upinzani.

January, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, alisema  hivi sasa kuna kazi kubwa ya kuendelea kuleta maendeleo ambayo yanahitaji umoja  na mshikamano.

Alisema migogoro, majungu na fitina inatokana na kambi  zilizokuwapo huku akiwasisitiza wana CCM watambue ni hema kubwa na linavumilia tofauti za watu.

Aliyekuwa  Mwenyekiti wa  Chadema  Kitongoji cha Kwemghogho, Shabani Kahema,  aliwataka   vijana  na  wanachama  wengine  kubadilika kwa kuwa CCM ndiyo chama chenye ilani inayotekelezeka.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sad.What makes the country strong, stable is the oppositions. What I can say is Tanzania is yet to learn from other countries. You cant allow one party, same people rule for more than fifty years. There is something very wrong with the education system in the country. People are still sleeping till everything is gone, It will be too late then.
    Sad Day.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umechemka!Una lengo la kumuelimisha kila M-TZ kweli?Yule mmasai kule kijijini ataelewa ulichoandika hapa?

      Delete
  2. Ongea kiswahili tu ndugu yangu

    ReplyDelete
  3. May be in the books, or advanced democracies. In reality, especially in Africa, opposition means oppose anything and everything. It is not about political ideology either, as witnessed by same people changing parties like changing lanes in highways. Look at how undemocratic-within opposition parties are in Tanzania for example!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad