Wananchi katika Wilaya ya Kwimba wamelazimika kumsimamisha Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kutokana na tishio la baa la njaa kutokana na mazao kukauka kwa ukosefu wa mvua.
Wakiwa wamemsimamisha Mkuu huyo wa Mkoa huku wakiwa wamebeba mabuwa ya mahindi yaliyokauka, walisema:-
"Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa, siyo kwamba watu hawajalima, wamelima sana lakini mazao yamekauka kutokana na ukame wa mvua.
Kipindi mvua zikinyesha, ukipita hapa ungeona watu wakitafuna mahindi ya kuchoma barabarani,lakini sasa hatuna namna,mazao yote yamekauka".
Kwa upande wake, RC Mwanza amesema atatuma timu ya Mkoa ili ilishirikiane na Wilaya ili waandae ripoti ya hali halisi iliyopo.